top of page
pexels-sergey-pesterev-8427984.jpg

Karibu 

Tujifunze kwa kutalii kwetu na nje ya nchi!

Tanzania Appointments, Roving Africa Safaris na Inspire Network inawakaribisha watanzania wote wenye mahitaji ya kufanya utalii kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali nchini au nje ya nchi kuwasiliana nasi na kuona jinsi tutakavoweza kusaidiana kuhakikisha hitaji lako linatimia kwa gharama nafuu. Tunahudumia makundi tu na si mtu mmoja mmoja katika kuduma hizi. 

​

Ndani ya Tanzania tunashirikiana na Roving Africa Safaris kukaribisha watanzania ambao wana mahitaji ya kuona mambo mbalimbali pamoja na kujifunza  tamaduni zetu. Gharama za kuhudhuria utalii huu zinategemea na muda na mahitaji ya wateja wetu. Lakini ni kati ya shilingi za kitanzania laki 5 na milioni moja kwa kila muhudhuriaji. Tafadhali jaza fomu hii hapo chini na utueleze mpango wako ili tuwasiliane nawe kwa maelezo na uhakiki wa ratiba na mengineyo. Tunatarajia kuwa kila anaewasiliana nasi atakuwa ni mtu mwenye group ya watu 8 au zaidi. 

​

Nje ya Tanzania tunakaribisha wanafunzi wa ngazi zote na vikundi vya wanajamii kujiunga na Inspire knowledge tours. Tunaweza kuandaa safari za kuja Scandinavian countries au nchi nyingine za Ulaya, Carribbean au nchi mbalimbali za Africa. Kama una group ambalo utapenda lijiunge na safari ya kimafunzo mahali popote  tujulishe kwa kupitia  fomu hii ya Inspire knowledge tours. Gharama za safari hizi za nje kwa wiki moja ni kuanzia US dollars 1600 (malazi, chakula, usafiri wa ndani). Pia utahitaji gharaa za ziada kwa ajili ya malipo ya visa, nauli za ndege na bima za kusafiria. Ili kuwa na uhakika wa kufanya safari kama hii iwezekane tunashauri kila mtu awe na US dollars 3000 (makadirio). 

pexels-sergey-pesterev-8427984_edited.jpg

Karibu. Tueleze mpango wako na tutawasiliana nawe kwa mpangilio zaidi

Tumia fomu hii hapa chini kwa utalii wa Tanzania

ROVING_AFRICA_FINAL_page-0001-removebg-preview.webp
logo white_edited.jpg

Asante kwa kujaza fomu hii. Tutawasiliana !

bottom of page